(ABNA24.com) Dk Mohammad Javad Zarif jana Jumatatu aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, wale wanaojidai ni mashujaa wa demokrasia wanapaswa kutambua kuwa, badala ya kung'ang'ania ndoto zao za kufanikisha Muamala wa Karne ambao utazaliwa ukiwa umeshakufa, wanapaswa kufuata njia ya utatuzi wa kidemokrasia iliyopendekezwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei nayo ni kuitishwa kura ya maoni ambayo itawashirikisha Wapalestina wote, Waislamu, Mayahudi na Wakristo ili wajiamulie wenyewe mustakbali wa nchi yao.
Mpango wa Muamala wa Karne uliopendekezwa na Marekani unajumuisha kukabidhiwa kikamilifu Israel mji mtakatifu wa Quds wenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa, vitongoji vilivyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan vyote ipewe Israel na Wapalestina wasiwe na haki ya kurejea kwenye ardhi za mababu zao.
Leo Jumanne, rais wa Marekani, Donald Trump amepanga kuuzindua mpango huo baada ya kuonana na waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu na Benny Gantz, mkuu wa Muungano wa Blu na Nyeupe wa utawala huo pandikizi.
/129